MCL Columnist

''Tutawakamata tu''

Print

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mecky Sadiki akiongozana na Mkuu wa Wilaya Kinondoni ,Jordan Rugimbana(kushoto)katika Mtaa Kinondoni  Mkwajuni kwenye operesheni maalumu ya kuwakamata wezi wa maji ya Kampuni ya maji ya Kusambaza Maji Safi katika jiji la Dar es Salaam(Dawasco)jana.Picha na Aika Kimaro

Sheria ziimarishwe kudhibiti ardhi

Print

Daniel Mwaijega
MOJA ya agenda moto inayotikisa Jumuiya ya Afrika Mashairi, ni haki ya wakazi wa nchi wanachama wa jumuiya hiyo kumilikishwa ardhi katika nchi mwanachama.

Kwa jumla, Tanzania ndiyo inaonekana kuwa kikwazo kwa kuwa inapinga hilo na wakati huohuo wananchi wake wana wasiwasi kuwa wakazi wa nchi nyingine, watawafunika katika nchi yao kwa kuwa kwa asilimia kubwa ni vigumu wao kwenda kupata ardhi Kenya au Uganda kutokana na ukweli kwamba imeshajaa.

Wizi huu wa madini yetu, halafu eti ‘kasungura kadogo’!

Print

Neville Meena
WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo ametufungua macho kwamba, kile ambacho kimekuwa kikipigiwa kelele kwa muda mrefu kuhusu wizi wa rasilimali za nchi yetu, kina ukweli ndani yake.
 
Kama habari ilivyoandikwa katika ukurasa wa kwanza wa gazeti hili inavyosomeka, ninafurahi kwamba kauli hii ya kukiri kuwepo kwa wizi wa kutisha kupitia utoroshaji wa madini na ukwepaji wa kodi, imetoka kwa Waziri wa Serikali.
 

 

Mnataka barabara za Magufuli zijengwe baharini?

Print

Julius Samwel Magodi
KAMA kuna jambo ambalo litatufanya Watanzania tusiendelee, tubaki tunalalamika tu wakati tuna kila kitu, ni viongozi wetu kutoheshimu utawala wa sheria.

Ukiona kiongozi wa familia hawezi kuheshimu sheria zilizotungwa kuongoza watu wake, ni wazi kwamba hata watoto nao hawataweza kuziheshimu.

 

 

Ukimwona tajiri tamani kuwa kama yeye, ukimwona maskini...

Print

Ndugu zangu,

JAMBO moja kubwa ni dhahiri kuwa Watanzania bado tuna safari ndefu sana kufikia hatua ya kuitwa taifa la kisasa. 
Tuyafanyayo mengi bado ni mambo ya hovyohovyo na wenye kuongoza kuyafanya hayo ya hovyohovyo ni viongozi wetu. Lakini hatuna jinsi, hatua tunayopitia sasa ni lazima tuipitie.

 

 

Nini kimesababisha tushindwe?

Print

TIDO MHANDO, LONDON
MICHEZO ya Olimpiki ya mwaka huu iliyoanza wiki mbili zilizopita kwa bashasha na vitimbi ambapo James Bond 007 alionekana akiwa bega kwa bega na Malkia Elizabeth wa Uingereza kwenye nderemo za ufunguzi, inafikia tamati kesho Jumapili.

Mataifa zaidi ya 200 yanashiriki kwenye michezo hii, mikubwa kuliko yote ulimwenguni inayoelezewa kuwa ndiyo kipimo cha ufanisi, ari na tashwishwi ya kila mwanamichezo duniani.

Inasemekana ya kwamba mwanasoka maarufu, David Beckham, licha ya yote makubwa aliyoyapata, bado alitamani kuwemo kwenye timu ya Uingereza ya Olimpiki, kunogesha kilele cha historia yake michezoni.

Kuachwa kwake kulimfanya asiwe na furaha kwa siku kadhaa hata kuwafanya waandaaji kumpatia nafasi ya kushiriki sehemu ya mwisho ya mbio za mwenge wa michezo hii.