Mwananchi Communications LTD BLOG

Mafunzo ya wanafunzi kwa vitendo

Print
User Rating:  / 0

Wanafunzi wa shule ya msingi Haydom Wilayani Mbulu Mkoani Manyara wakijifunza kutengeneza nishati ya mkaa mbadala kwenye Kituo cha pembe nne za utamaduni Haydom (4CCP) juzi kwa lengo la kutunza mazingira.Picha na Joseph Lyimo                             

''Tutafika mdogo mdogo''

Print
User Rating:  / 0

Daladala likipita katika njia inayoungnisha Kimara na Bonyokwa nje kidog ya jiji la Dar es Salaam jana, barabara hiyo iliyojengwa kwa kiwango cha changarawe na mifereji mwezi wa tatu kwa sasa inapitika kwa shida baada ya sehemu nyingi kuharibika kutoka na ujenzi kutozingatia utaalumu wa kutosha. Picha na Salhim Shao

''Hatutaki watalii!''

Print
User Rating:  / 0

Wananchi  wanaoishi ndani ya eneo la Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro katika kijiji cha Olbalbal wakiwa kwenye kikao walichokubaliana kuzuia watalii kuingia katika hifadhi hiyo kwa kufunga geti iwapo serikali haitatekeleza matakwa yao. Picha na Mussa juma

''hali sio nzuri''

Print
User Rating:  / 0

Mvuvi wa samaki kwenye Ziwa Bassotu, mkoa wa Manyara,Charles Manyama akizungumzia hali kipato chao kuyumba baada ya Ziwa hilo kufungwa kwa muda  ili kuwezesha samaki kuongezeka.Picha na Filbert Rweyemamu

Bungeni laendelea

Print
User Rating:  / 0

Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ali Kessy akiwa amefumba mdomo wakati bunge lilipokuwa limekaa kama kamati kupitisha makadirio na matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2013/14, mjini Dodoma jana. Kushoto ni Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe akifurahi wakati Kessy alipokuwa akifanya tukio hilo. Picha na Edwin Mjwahuzi

"Hongera Waziri"

Print
User Rating:  / 1

Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli (mwenye tai nyekundu) akipongezwa na wabunge pamoja na mawaziri baada ya kupitishwa kwa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2013/14, mjini Dodoma juzi. Picha na Edwin Mjwahuzi

"Pumzikeni kwa amani"

Print
User Rating:  / 0

Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada,John Baird(kushoto)akiweka shada la maua jana kwenye makaburi ya watu watatu waliouawa kwenye tukio la shambulio la bomu kwenye kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Parokia ya Olasiti,jijini Arusha Mei 5,mwaka huu.Picha na Filbert Rweyemamu

Faida za virutubisho katika vyakula

Print
User Rating:  / 0

Ofisa wa Lishe kutoka katika Sekta ya Maendeleo na Menejimenti za Afya, Leticia Chang’a akiwaelezea faida za virutubisho katika vyakula wakazi wa jiji la Dar es Salaaam walitembelea maonesho ya lishe jana  yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja. Picha na Venance Nestory

"Tunalinda mazao"

Print
User Rating:  / 0

Wakulima wa mpunga katika kijiji cha Mgungila mkoani Singida wakiwa kwenye lindo la kuwafukuza ndege ambao wamekuwa wakila mpunga huo, ambapo wamesema bila ya kulinda wanaweza kumaliza shamba lote.Picha na Masoud Masasi

Mkagangamale vijana

Print
User Rating:  / 0

Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi bendera kiongozi wa batalioni ya  wanajeshi wa JWTZ wanaokwenda  kujiunga na  jeshi la Umoja wa Mataifa la kulinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, katika sherehe za kuwaaga zilizofanyika Msangani, Kibaha, Mkoa wa Pwani  jana. Picha na Ikulu

Msaada wa blanketi

Print
User Rating:  / 0

Mbunge wa Kishapu mkoani Shinyanga Suleiman Nchambi akikabidhi blanketi kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokea katika Vijiji vitatu vya Mwanhili Mwasubi na Itongoitale katika kata  ya Bunambiyu Tarafa ya Mondo  wilayani Kishapu.

Uzinduzi wa ilani ya madai kwa wanawake

Print
User Rating:  / 0

Wananchi wakiwa katika maandamano  jana   kabla ya uzinduzi wa ilani ya madai ya wanawake wa Tanzania katika katiba mpya  iliyotayarishwa na Mtandao wa Jinsia  Tanzania(TGNP) jijini Dar es salaam. Picha na Aika Kimaro      

Ulinzi mkutanoni

Print
User Rating:  / 0

Wakazi wa manispaa ya Singida mkoani humo wakimsikiliza katibu mkuu wa chama cha CUF,Seif Sharrif Hamad katika mkutano wa hadhara uliofanyika juzi.Picha  na Gasper Andrew.

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknollojia

Print
User Rating:  / 0

Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknollojia, Prof. Makame Mbarawa akiongea na mmoja wa wajasiliamali kwenye semina iliyoandaliwa na Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) chini yaTume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na taasisi ya GIST ya Marekani kwa ajili ya kuwapa mbinu mbalimbali za kijasiliamali. Picha na Rafael Lubava

Balozi wa Marekani

Print
User Rating:  / 1

Balozi wa Marekani nchini, Alfonso E. Lenhardt akizungumza kwenye semina ya wajasiliamali

Mkurugenzi Mkuu waTume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH)

Print
User Rating:  / 0

 

Mkurugenzi Mkuu waTume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) Dr. Hassan Mshinda akizungumza kwenye semina  ya siku mbili kwa ajili ya wajasiliamali iliyofanyika jijini Dar es Salaam jana.

Semina ya ujasiliamali

Print
User Rating:  / 0

wajasiliamali mbalimbali wakifuatilia semina Iliyoandaliwa na Dar Teknohama Business Incubator (DTBi) chini yaTume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) kwa kushirikiana na taasisi ya GIST ya Marekani. Picha na Rafael Lubava

Tunakoelekea.........!

Print
User Rating:  / 1

Majeruhi wakiwa kwenye hospitali ya mkoa wa Mount Meru wakipata matibabu kutokana na kushambuliwa na mtu asiyejulikana na kitu kinachosadikiwa ni Bomu la kurushwa kwa mkono wakati waumini hao walipokuwa kwenye ibada ya uzinduzi wa Kanisa Katoliki Parokia ya Mtakifu Joseph Mfanyakazi,Jimbo Kuu la Arusha jana. Mtu mmoja amefariki na 61 kujeruhiwa. Picha na Filbert Rweyemamu

Viatu vya watu waliopata madhara ya mlipuko wa bomu

Maafisa wa Polisi wakichunguza milipuko kwenye eneo la Kanisa

Mtoto aliyejeruhiwa akipata matibabu

Jengo la Kanisa la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi,Jimbo Kuu la Arusha lililokuwa lizinduliwe jana na Balozi wa Vatican na Mjumbe Maalumu wa Papa,Askofu Mkuu,Fransis Padilla. Shughuli hiyo ilisitishwa baada ya mtu asiyejulikana kurusha kitu kinachosadikiwa ni Bomu na kuua mtu mmoja na kujeruhi 61.



Maadhimisho ya Albino

Print
User Rating:  / 0

Wananchi wakishiriki kwenye maandamano ya kilele cha maadhimisho ya siku ya walemavu wa ngozi (albino) yaliyofanyika mkoani Singida juzi. Picha na Gasper Andrew 

Kufa kupona

Print
User Rating:  / 0

Mshambuliaji wa Atletico Madrid raia wa Kolombia, Radamel Falcao (katikati) akigombania mpira na winga wa Real Madrid, Kaka (kushoto) na beki, Ricaldo Calvalho kwenye mechi ya ligi kuu ya Hispania katika uwanja wa Vicente Calderon, Madrid juzi, Real Madrid ilishinda 2-1. Picha na AFP

Madhara ya vurugu

Print
User Rating:  / 0

Wakazi wa Liwale, wakiondoa mabaki ya dawa za kilimo mali ya Makamu Mwenyekiti wa chama cha msingi cha Umoja,Hasani  Mpako, zilizoteketezwa kwenye nyumba yake, wakati wa vurugu zilizotokea wiki iliyopita, watu 31 wanatarajiwa kufikishwa mahakamani leo, kujibu tuhuma kuhusiana na vurugu hizo. Picha na Christopher Lilai

Kibaka

Print
User Rating:  / 1

Wanausalama wakimdhibiti kijana anayedaiwa kuwa ni kibaka,  baada ya kumkwapulia simu  abiria aliyekuwa ndani ya daladala wakati likitembea, mjini Morogoro jana. Uporaji umekuwa ukiongezeka siku hadi siku hasa katika maeneo ya mijini. Picha na Juma Mtanda

Taka barabarani

Print
User Rating:  / 0

Taka zikiwa zimelundikwa katika barabara inayojengwa ya mradi  wa Mabasi yaendayo Kasi (DART), eneo la Magomeni Kagera  Dar es Salaam jana. Mradi huo umekuwa ukikumbana na changamoto nyingi ikiwa ni pamoja na machinga kuvamia eneo la mradi na  uhalibifu wa miundombinu unaofanywa na  madereva wanaokwepa foleni.  Picha na Venance Nestory

Msaada wa madawati

Print
User Rating:  / 0

Mwananfunzi wa darasa la tau wa shule ya msingi Misuna ya Singida, Athumani Jingu  na Mkuu wa mkoa wa Sindida, Dk.Parseko Kone (kushoto) wakipoea sehemu ya madawati  264, kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) Nehemia Mchechu wa pili (katikati), na makamu mwenyekiti wa  Hassan Maajar Trust (HMT), Shariff Maajar (wa pili kulia),  kwenye hafla iliyofanyika mjini Singida, Madawati yaliyotolewa na NHC. Kulia ni Ofisa balozi Bertha Sami. Picha na Gasper Andrew.

Buriani Bi Kidude

Print
User Rating:  / 0

Msanii mkongwe wa nyimbo mbalimbali zikiwemo za asili, Fatma binti Baraka 'Bi Kidude' amefariki jana mara baada ya kusumbuliwa na maradh mbalimbali kwa muda mrefu.

Heshima za mwisho

Print
User Rating:  / 1

 

Viongozi na wananchi wakiwa wamesimama mbele ya jeneza lililokuwa na mwili wa Mkuu wa zamani wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) Meja Jenerali Makame Rashid, Makao makuu ya Jeshi hilo Mlalakuwa Dar es Salaam, kabla ya  za mwisho  jana. Picha na Rafael Lubava                     

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (JWTZ) Davis Mwamunyange akitoa heshima za mwisho

Print
User Rating:  / 0

Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi nchini (JWTZ) Davis Mwamunyange akitoa heshima za mwisho kwenye jeneza lililokuwa na mwili wa Mkuu wa zamani wa Jeshi la Kujenga Taifa(JKT) Meja Jenerali Makame Rashid, Makao makuu ya Jeshi hilo Mlalakuwa Dar es Salaam, jana. Picha na Rafael Lubava                     

Adha ya upanuzi wa barabara

Print
User Rating:  / 0

Wakazi wa Mianzini, mkoani Arusha wakipita kandokando ya nyumba zilizokuwa zikivunjwa ili kupanua barabara ya Mianzini hadi Sambasha yenye urefu wa kilomita 19. 7. Picha na Moses Mashalla

Lori lamlazimisha mwananchi kukaa banda

Print
User Rating:  / 0

Lori likiwa  limeparamia migomba na kupinduka wilayani Ngara, Mkoani Kagera na kujeruhi watu kadhaa na kuharibu nyumba ya Bibiana John ambaye amelazimika kukaa katika banda la muda. Picha na

Ajali ya ndege yamuua Bob Sambeke

Print
User Rating:  / 1

Wananchi wakiangalia ndege aina ya Cessna 5H-QTT ikiwa imeanguka eneo la Kisongo, karibu na Uwanja wa ndege wa Arusha juzi, baada ya kugonga mti wakati ikijiandaa kutua na kusababisha kifo cha mmiliki wake na aliyekuwa rubani, Bob Sambeke. Picha na Filbert Rweyemamu                                                               

Msaada kwa wananchi

Print
User Rating:  / 0

Wananchi wa vijini vya Itongo itale na  Mwanhili Wilayani Kishapu, Mkoani Shinyanga, waliokumbwa na maguriko na kupoteza nyumba, vyakula na mifugo, wakimsikiliza mkuu wa mkoa  Ally Rufunga alipowatembelea na kutoa ahadi ya sh16.6 za kuwasaidia. Picha na Suzzy Butondo                     

Chanjo ya mbwa

Print
User Rating:  / 0

Afisa Mifugo wa Kata ya Ukonga Fatuma Hassan, akitoa chanjo ya kichaa cha mbwa katika Kata ya Msongola, Ilala Dar es Salaam juzi, ili kudhibiti ugomjwa huo unaombukizwa kutoka kwa mbwa kwenda kwa binadamu, endapo atang’atwa na mnyama mwenye ugonjwa. Picha na Pamela Chilongola 

Sala ya mazishi

Print
User Rating:  / 0

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Idara ya Wanyamapori, Muhidin Ndolanga (kushoto) akishiriki kisomo cha kumwombea Marehemu Meja Jenerali Makame Rashid ambaye  aliwahi Mkuu wa Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) na  Balozi  wa Tanzania nchini Malawi aliyefariki jana Dar es Salaam. Anatarajiwa kusafirishwa kwenda kuzikwa wilayani Tandahimba baada ya taratibu zote za kuaga kukamilika.Picha na Salhim Shao

Gesi asilia

Print
User Rating:  / 0

Mwenyekiti wa  Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF), Prof. Ibrahim Lipumba, akiwakilisha mada  kuhusu gesi asilia wakati wa  kongamano la Chama hicho,  mjini Mtwara juzi. Picha na Abdallah Bakari

Gari juu ya mkokoteni

Print
User Rating:  / 0

Wakazi wa mjini Singida, wakijaribu kuongoza  mkokoteni unaonekana kuwashinda  nguvu wakati wakihamisha bodi ya gari kama walivyokutwa jana. Picha na Gasper Andrew   

Rais na raia wake

Print
User Rating:  / 0

Rais Jakaya  Kikwete akisalimiana na wananchi wa Kijiji cha Kasera Wilayani Mkinga, Mkoani Tanga,  baada ya kuzindua  mpya ya rami yenye urefu wa km 60 kutoka Tanga hadi Horohoro, mpakani mwa Kenya,  iliyojengwa ufadhili wa mfuko  Marakeni wa Millennium Challenge Corporation (MCC). Picha na Salim Mohammed

BAKWATA YAUNGA MKONO UCHINJAJI

Print
User Rating:  / 0

Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salim akiongea na waandishi wa habari jijini hapa jana kuhusiana na mambo mbalimbali yaliyojitokeza na kuhatarisha amani na kusema ili kuyaepusha ni vizuri viongozi wa dini kukutana mara kwa mara. Picha  na Rafael Lubava

 

BAKWATA YAMUUNGA MKONO MWINYI

Rafael Lubava. Mcl blog

Balaza Kuu la Waislam nchini (BAKWATA) limeunga mkono  kauli ya Rais wa awamu ya pili, Ali Hassan Mwinyi kuhusiana na uhuru wa kuchinja na kusema ni vizuri kufuata utaratibu uliokuwepo kwani hauna kasoro ili kudumisha amani.

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Sheikh Mkuu wa Mkoa wa huu, Alhad Mussa Salim alisema ni vizuri kufuata utaratibu wa mtu kujichinjia kinachotumika na familia lakini kama cha jamii kwa ujumla ufuatwe ule wa zamani.

‘’Mkristo ajichinjie anachotaka ale vile vile na Muislamu naye afanye hivyo kwa kile kinacholiwa kifamilia, lakini kama ni kwa ajili jamii nzima, jamani tuendelee tu kufuata tu utaratibu uliopo’’ Alisema na kuongeza.

‘’Mkristo hana mwiko kula kilichochinjwa na Muislamu na ndivyo ilivyokuwa miaka yote ambapo nyama inayotakiwa itumike na jamii imekuwa ikichinjwa na Waislamu na tumeishi hivi bila shida yoyote kwa miaka yote’’

Pamoja na hayo Sheikh Salim alisema tatizo kubwa linalosababishwa uwepo wa migogoro nchini ni kutokutana mara kwa mara kwa viongozi wa dini ili kujadili na kutatua tofauti zao kabla hazijaeta madhara.

‘’Viongozi hawakutani mpaka migogoro itokee, hivyo hata kama kuna vuguvugu za chini kwa chini ni vigumu kujua, unakuja kugundua tayari hali ni mbaya na inakuwa ni vigumu sana kurejesha amani mapema’’.

Alimsifu pia Rais Jakaya Kikwete kwa taarifa yake ya mwisho wa mwezi na kusema ilikuwa na lengo la kuleta utulivu na amani japo kulikuwa na lawama kutoka kwa baadhi ya Wakristo na Waislamu.

‘’Kwa kweli ilikuwa na manufaa sana kwa Taifa tofauti na wengine walivyoichukulia, Rais hakupendelea upande wowote, ila lengo lake ni kuona watu wake wanaishi kwa amani’’.

Pia alimuomba Sheikh Mkuu wa Tanzania, Mufti Shaban Bin Simba kuharakisha uteuzi wa jopo la wawakilishi kwa ajili ya kukutana na Wakristo ili kujadili na kutafuta suluhu ya hali iliyopo nchini kwa sasa.

Kwa siku za karibuni kumekuwa na migogoro mbalimbali nchini ya kidini kati ya Wakristo na Waislamu huku kila upande ukisema sababu zake na kusababisha amani kwa baadhi ya maeneo kuyumba.

Wakuu wa mikoa Bungeni

Print
User Rating:  / 0

Wakuu wa mikoa wakisoma hotuba ya bajeti ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2013/14 ilipokuwa ikiwasilishwa bungeni juzi. Picha na Edwin Mjwahuzi

Biashara barabarani

Print
User Rating:  / 0

Wanyabiashara ndogondogo wakiwa wamepanga bidhaa zao katikati ya barabara ya Morogoro eneo la Manzese jijini Dar es Salaam kitu ambacho kimekuwa kikilalamikiwa na wakandrasi  wa barabara hiyo kutokana na uharibifu wa baadhi ya miundombinu hiyo. Picha na Fidelis Felix

Hizi nayo!

Print
User Rating:  / 0

Wananchi wakiangalia gari iliyotumbukia katika mtaro kando ya barabara ya Mandela karibu na ofisi za Mwananchi Communications Ltd (MCL) Dar es Salaam jana. Picha na Salhim Shao

Usafiri ziwani

Print
User Rating:  / 0

Wakazi wa Mwamboa wa Ziwa nyasa Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe wakivuka katika ziwa hilo kwa kutumnia usafiri wa Mtumbwi.  Picha na Said Ng'amilo.

Tuyapende mazingira yetu

Print
User Rating:  / 0

Mkazi wa Kijiji cha Ndembo, Halmashauri ya Busokelo, wilayani Rungwe, Mbeya, akifanya usafi wa mazingira katika Soko  la kijijini  chao.

Usafi wa mazingira ni kitu cha lazima ili kuyaweka safi na kuepuka na hatari ya kupata magonjwa mbalimbali. Picha na  Godfrey Kahango

''Tupendane jamani''

Print
User Rating:  / 0

Katika jamii tunatofautiana kwa vitu vingi ikiwa ni pamoja na utofauti wa kipato, akili, uwezo wa kufanya kazi na kadharika. Inawezekana ni mpango wa Mungu ili tuweze kutumikiana kwa yeye mwenyewe anasema, ''huwezi kumpenda Mungu usiyemuona na kumchukia binadamu unayemuona

Tunahimizwa kupendana na kusaidiana kwa hali na mali na zaidi kwa wale wanaoonekana wanahitaji huruma hiyo zaidi.

''Hongera Uhuru''

Print
User Rating:  / 0

Rais Jakaya Kikwete akimpongeza Uhuru Kenyatta kabla ya kuapisha jijini jana kuwa rais wa nne wa nchi hiyo. Katikati ni Naibu Rais wake, William Ruto. Picha na Mpiga Picha wetu. Nairobi

''Nitailinda nchi''

Print
User Rating:  / 1

Rais wa awamu ya nne wa Kenyas  Uhuru Kenyatta akionyesha upanga aliopokea kama nembo ya Taifa hilo kutoka kwa Rais anayemaliza muda wake Mwai Kibaki (kushoto) kwenye sherehe za kuapishwa kwake katika viwanja vya Moi International Sports Center Kasarani, Nairobi jana. Uhuru Kenyatta. Picha na AFP 

Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja, akijaribu moja ya magari aliyoyazindua

Print
User Rating:  / 0

Mkuu wa Jeshi la Magereza nchini, Kamishna Jenerali John Minja, akijaribu moja ya magari aliyoyazindua kuashiria uzinduzi wa kuwasafirishia Mahabusu kwenda Mahakamani  kwa Mkoa wa Dodoma. Uzinduzi huo ulifanyika katika Gereza Kuu Isanga Dodoma jana. Picha na Felix Mwagara

Mchakato wa Katiba mpya kwenye asasi ya AFL

Print
User Rating:  / 0

Mkazi wa Ilomba Ilomba Jijini Mbeya, Ruth Green, akisoma baadhi ya vifungu vilivyomo ndani ya katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania mara baada ya asasi isiyokuwa ya kiserikali ya Aman The Foudation Of Life (AFL) Kuwagawia katiba hizo walipofika katika kanisa na Baptist jana. Picha na Godfrey Kahango         

Ukuta wa RTD wabomolewa

Print
User Rating:  / 0

Wapita njia wakishangaa ukuta wa Radio Tanzania Dar es Salaam (RTD)  uliovunjwa na Wakala wa barabara Tanroad katika eneo la Tazara jijini Dar es Salaam jana na kufanya kazi ya ulinzi wa eneo hilo nyeti, kuwa ngumu. Picha na Venance Nestory

Utendaji kazi waWizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo.

Print
User Rating:  / 0

Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein, akizungumza na Uongozi wa Wizara  ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo,katika utekelezaji wa kazi za Wizara hiyo, Ikulu Mjini Zanzibar jana kwa ajili ya kuhakikisha huduma zitolewazo na wizara hiyo zinawasaidia ipasavyo wananchi. Picha na Mpiga Picha wetu

Msaada kwa wagunduzi na wajasiliamali nchini

Print
User Rating:  / 0

Rafael Lubava, Mcl blog

Tume ya Sayansi na Teknolojia imetoa mfano hundi kwa wagunduzi na wajasiliamali sita wa Teknolojia Habari na Mawasiliano (TEHAMA) zenye dhamani ya Tsh 82 milioni kwa wajasiliamali ili kuwasaidia kuendeleza shughuli zao walizoanzisha

Hundi hizo zilikabidhiwa na Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa makao makuu ya COSTECH jijini Dar es Salaam jana baada ya kushinda mchakato uliokuwa na zaidi ya wajasiliamali 30 waliotuma maombi yao.

Profesa Mbarawa alisema msaada huo umetolewa ili kuwapunguzia changamoto wanazokabiliana nazo ikiwa ni pamoja na kutokuwa na mitaji mikubwa, kutokuwa na vigezo vya kutosha kuomba mikopo na vitendea kazi vya kisasa.

‘’Changamoto zenu ni nyingi na Serikali kwa kutambua hilo, imetoa pesa hizo ili kuwasaidia kuendeleza ujasiliamali na ugunduzi wenu na hatimaye muweze kuwasaidia Watanzania wenzenu pia mvuke mipaka kama wengine’’. Alisema hayo na kuongeza.

Serikali imetenga Tsh bilioni 1.2 kwa  ya kusaidia mfuko wa wabunifu wa sayansi na mawasiliano, mchakato mwingine utafanyika ili na wengine waweze kupata msaada utaowawezesha kufikia malengo yao’’.

Naye Mkurugenzi  Mtendaji wa DTBi, Mhandisi George Mulamula amesema wajasiliamali na wabunifu wa hapa nchini ni lazima wawezeshwe kwa ajili ya manufaa ya Taifa na kuongeza ushindani wa Kimataifa.

‘’Wengi wao uwezo wao kifedha ni mdogo lakini wa uwezo kigunduzi wa vitu mbalimbali, ndio maana tumeanzisha mfuko utakaowasaidia katika tafiti zao ili kuhakikisha uwezo wao unatumika vizuri na kuleta manufaa kwa nchi nzima.

Wajasiliamali hao wameishukuru COSTECH na Serikali kwa msaada huo na kuahidi utatumika kama ilivyo pangwa kwa kuwa mtaji hawakuwa na fedha za kutekeleza shughuli zao.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa hundi hiyo, Dickson Ng’ang’a  amesema inawezekana hata wao kuwa wajasiliamali wakubwa kama watapewa ushirikiano wa kutosha na kushauri ni vizuri kuwa waaminifu kwa msaada wanaopewa kuutumia kama ilivyokusudiwa.

Mfuko huo wenye lengo la kuwakwamua wajasiliamali nchini ili kuwasaidia kupata mahitaji mbalimbli ya kifedha na elimu, mbali na Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia, mfuko huo unafadhiliwa pia na Wizara ya Mambo ya Nje ya Finland.

Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Profesa Makame Mbarawa akikabidhi mfano wa hundi kwa mjasiliamali na mgunduzi Mustapha Suleiman yenye thamani ya Tsh16 milioni kwa ajili ya kumsaidia katika shughuli zake. Picha na Rafael Lubava

                         

 

 

Mtafutaji hachoki

Print
User Rating:  / 0

Mwanamke wa jamii ya wafugaji akisuka mapambo ya shanga kwa ajili ya kuwauzia mbalimbali. Mama huyo pia huuza dawa za kienyeji katika eneo la Magomeni Kanisani jijini Dar es Salaam jana.Picha na Silvan Kiwale

''Hii ni kwa ajili ya masomo jamani''

Print
User Rating:  / 0

Naibu waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Philipo Mulugo akizindua tovuti iitwayo www.shuledirect.co.tz jijini Dar es Salaam jana itakayosaidia wanafunzi wa sekondari kujifunza na kubadilishana ujuzi na wenzao kwa kutembelea tovuti hiyo. Wanaoshuhudia ni wanafunzi wa shule ya sekondari Kisutu.Picha na Silvan Kiwale

''Utajieleza kituoni''

Print
User Rating:  / 0

Askari Polisi wa Kituo cha Polisi Buguruni akimwadhibu kijana ambaye haikujulikana kosa lake mbele  ya  Ofisi ya Upelelezi Mdogo na Dawati la Jinsia na Watoto baada ya kufikishwa katika kituo hicho jijini Dar es Salaam jana.Picha na Fidelis Felix

''Tulia''

Print
User Rating:  / 0

Askari Kanzu wakimlinda kibaka aliyepewa kipigo na wananchi jana katika eneo la Buguruni Ghana baada ya kutenda uhalifu. Vibaka wamekuwa wakihatarisha maisha ya watu na mali zao kitu ambacho huleta kero sana. Picha na Venance Nestory

Ghai ''Nazindua''

Print
User Rating:  / 0

Mwandamizi wa Katiba Institute ya Kenya, Yash Ghai akikata utepe mbele ya wajumbe wa kamati maalum ya katiba inayoratibiwa na kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) kwenye uzinduzi wake uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kamati hiyo itakuwa na shughuli mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa watu kuhusiana na nchakato huo. Picha na Rafael Lubava

Kamati maalum ya katiba inayoratibiwa na kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC)

Print
User Rating:  / 0

Mwenyekiti wa kikao cha kamati maalum ya katiba inayoratibiwa na kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Jenerali Ulimwengu akifafanua jambo wakati wa mkutano wa uzinduzi wake uliofanyika jijini Dar es Salaam jana. Picha na Rafael Lubava

Bilal atembelea Tume ya Sayansi

Print
User Rating:  / 0

Nora Damian,MCL

Dar es Salaam.Makamu wa Rais Dk Mohamed Gharib Bilal ameitaka Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) kutumia wataalamu wa ndani kwa ajili ya kufanya tafiti zitakazosaidia nchi kuwa ya kisasa hasa katika fani za viwanda, tiba na kilimo.

Akizungumza jana baada ya kutembelea tume hiyo, Dk Bilal alisema serikali itaendeea kuongeza juhudi ili kuzalisha wataaamu wengi wa sayansi na teknolojia kwa ajili ya kuleta maendeleo.

Aliipongeza tume hiyo kwa kutoa ufadhili wa masomo ya elimu ya juu kwa wanafunzi 219 kwani hatua hiyo itasaidia kuongeza idadi ya wataalamu na kuwa na soko la ajira lenye tija.

“Tunatambua mchango mkubwa unaofanywa na Costech ili kuhakikisha nchi inapata wataalamu wengi wanaohusika na mambo ya sayansi na teknolojia,”alisema Dk Bilal.

Alisema kuna fursa nyingi ambazo hazikuwepo miaka ya nyuma lakini hivi sasa zinawea kutumiwa kutatua matatizo yaliyoko na kujiendeleza kiuchumi.

Awali Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Kuendeleza Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kilicho chini ya tume hiyo (DTBi) George Mulamula, alisema tangu kuanza kwa kituo hicho wamefanikiwa kujenga uwezo wa ndani na kutatua matatizo ya Watanzania katika teknolojia hiyo na kupunguza mzigo wa kibiashara kwa kampuni change.

Hata hivyo alisema wanakabiliwa na changamoto kadhaa zikiwemo ukosefu wa mitaji ya kutosha kwa wajasiriamali, garama kubwa za vifaa vya mawasiliano na fikra potofu za baadhi ya vijana kutaka kuajiriwa badala ya kujiajiri wenyewe.

 

Dk. Bilal akiangalia moja ya vitabu vya wadau

 

Dk. Bilai akipata ufafanuzi wa jambo,katikati ni Mkurugenzi wa COSTECH, Hassan Mshinda

 

Mkurugenzi wa Vera Lab,(mwenye nguo nyekundu) akimweleza Makamu wa Rais, Dk. Gharib Bilal jinsi wanavyotoa huduma kwa shule zisizo na maabala kupitia huduma hiyo ilyopo kwenye gari.

Wadau wakifuatilia mtutano. Picha zote na Rafael Lubava

Mafundi TTCL

Print
User Rating:  / 0

Mafundi wa kampuni ya simu ya TTCL wakiunganisha nyaya zilizokatwa kwa bahati mbaya na wafanyakazi wa kampuni ya ujenzi ya Strabag wakati wakichimba mtaro wa maji machafu katika eneo la Ubungo jijni Dar es Salaa.

Mkutano COSTECH

Print
User Rating:  / 0

 

 

Nora Damian,MCL

Dar es Salaam.Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech) imepata msaada wa zaidi ya Sh 400 milioni kutoka kampuni ya Technobrain ambayo inajihusisha na masuala ya teknolojia ya habari na mawasiliano kwa ajili ya kukuza ujasiriamali na ubunifu.  

Fedha hizo zimetolewa kupitia kituo cha kuendeleza teknolojia ya habari na mawasiliano (DTBi) ambacho kiko chini ya tume hiyo.

Akizungumza jana wakati wa kusaini makubaliano hayo, Mkurugenzi Mkuu wa Costech, Dk Hassani Mshinda, alisema fedha hizo Dola 30,000 za Marekani zitasaidia wajasiriamali ambao wana makampuni yao ili yaweze kukua zaidi na kufanya kazi kwa ubora.

“Kuna vijana wengi ambao hawana mitaji wala ujuzi katika masuala mbalimbali hasa yanayohusu Tehama hivyo fedha hizi zitasaidia kupanua shughuli za DTBi ili ziweze kuwafikia watu wengi zaidi,”alisema Dk Mshinda.

Awali Ofisa Mtendaji Mkuu wa (DTBi) George Mulamula, alisema tangu kuanzishwa kwa kituo hicho hadi sasa wamefanikiwa kutengeneza ajira 4,500.

Pia alisema wameanzisha mfuko wa fedha wa kusaidia wajasiriamali na kwamba hadi sasa wameshapata Euro 100,000.

Alisema kupitia program mbalimbali zinazoendeshwa katika kituo hicho wameweza kusaidia vijana kuandika program ndogondogo kwenye simu kuhusu masuala ya afya, kilimo na biashara ambazo zimeonyesha mafanikio makubwa kwa sababu simu za mkononi zinatumiwa na watu wengi.

Mkurugenzi Mkuu wa COSTECH, Hassan Mshinda akiongea kwenye mkutano.

Wajumbe wakiteta jambo wakati wa mapumziko mafupi

Wajumbe wa mkutano wakifuatilia mambo mbalimbali kwenye mkutano.

Haya ndio maisha yetu

Print
User Rating:  / 2

 

Maisha yana tofauti sana kutoka familia moja hadi nyingine, wakati wengine wakiwa hawana uhakika wa kula ,wengine wanakula na kusaza wao na mifugo yao, tena kuna familia nyingine husikia tu masuala ya kwenda katika hoteli kubwa kubwa.

Hali hiyo haikwepeki katika nchi yoyote duniani,lakini ni vizuri kuwa na huruma ya kujali wengine wasio nacho ili nao wajione wana haki ya kuishi.

Picha hizi zinaonyesha tofauti ya maisha kati ya watoto wa wenye uwezo na wasio nao.

watoto wakicheza kwenye chombo maalum cha michezo

Watoto wa mitaani wakiomba msaada abiria walioko kwenye daladala. Picha zote na Rafael Lubava

More Articles...

  1. Mahafari ya DSJ

Wanaoperuzi SASA!

We have 12 guests and no members online

Banner One

Popular Blogs