Mwananchi Communications LTD BLOG

ABIRIA WANUSURIKA KIFO

Print
User Rating:  / 28

Abiria wakishuka kwenye kivuko cha Mv Magogoni katika eneo la Kigamboni jijini Dar es Salaam jana baada ya kuanza safari baada ya kupata hitilafu juzi.Picha na Michael Jamso

TUME CHOKA UHARIBIFU WA MISITU

Print
User Rating:  / 1

Mkazi wa kijiji cha Namatumbusi wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi Rashidi Mtambo akilalamikia ushirikishaji mdogo wa jamii katika kutunza na kuhifadhi misitu ya asili ya vijiji na mpango wa matumizi bora ya ardhi kwenye mkutano wa wadau wa misitu ulioandaliwa na shirika la kuhifadhi mipingo kwenye mradi wa mama misitu uliofanyika jana.Picha na Mwanja Ibadi

USALAM BARABARANI

Print
User Rating:  / 6


Askari wa usalama barabarani koplo Charles akimpima  ulevi dereva wa basi la al-saed Festo Gama kupitia kipimo maalumu wakati wa operesheni maalum ya kuwabaini madereva walevi na makosa mbalimbali kwenye mabasi.Kushoto ni afisa mfawidhi wa sumatra mkoa wa morogoro Luhamba Walukani. Picha na Hamida Shariff

MKE WA RAIS AKIHUTUBIA

Print
User Rating:  / 2

Mke wa Rais,Mama Salma Kikwete akionyesha Tuzo ya Heshima ya kutambua mchango wake kama kiongozikatika kutetea wanawake ya mwaka 2013(The Global Insparational Leadership Award )aliyopewa katika nchin za Falme za Kiarabu jijini Dar es Salaam jana.Picha na Fidelis Felix

BUNGE LIKIENDELEA

Print
User Rating:  / 13

Naibu Waziri, Ofi si ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, (TAMISEMI), Aggrey Mwanri (kushoto), akizungumza na Mbunge wa kuteuliwa Dk Asha Rose-Migiro(kulia) na Mbunge wa Viti Maalum Ritta Mlaki, bungeni Dodoma jana.Picha na Emmanuel Herman

HILI NDO BWAWA LETU

Print
User Rating:  / 0

Balozi wa Japani nchini, Mafaki Okada (watatu kushoto) akipewa maelezo na Afisa kutoka Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Juma Bakari (wapili kushoto) alipotembelea bwawa la kuvuna chumvi lililopo Shenge Juu, mkoa wa Kaskazini Pemba. Na Mpigapicha Wetu

TUPO KWAJILI YENU

Print
User Rating:  / 1

Baadhi ya wahudumu wa vituo mbalimbali vya afya mkoani Rukwa wakishiriki mafunzo ya kuboresha viwango vyao vya elimu ya masuala ya afya kupitia mradi wa wazazi na mwana unaotekelezwa na mashirika ya Plan International, Africare na Jhpiego. Picha na Mussa Mwangoka

TUTA FIKA TU!!

Print
User Rating:  / 1

Mwendesha bodaboda akiwa amepakia abiria watatu kwenye chombo hicho cha usafiri, jambo ambalo ni hatari kwa usalama wao, kama walivyokutwa eneo la Mwembeyanga, jijini Dar es Salaam juzi.  Picha na  Joseph Zablon

HALI TETE UBUNGO

Print
User Rating:  / 2

Abiria wakisubiri usafiri kwenye kituo cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo, baada ya kuambiwa gari lililotakiwa kuwapeleka mkoani Mbeya lilikuwa alijafika kituoni hapo. Picha na Fidelis Felix

TUTETE KIDOGO

Print
User Rating:  / 0

Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai (kushoto) akizungumza na Mbunge wa Lindi Mjini (Cuf), Salum Barwany kwenye Viwanja vya Bunge, mjini Dodoma jana. Picha na Emmanuel Herman

NAOMBA MUONGOZO

Print
User Rating:  / 3

Mbunge wa Iramba Magharibi (CCM), Mwingulu Nchemba akiomba mwongozo kwa Naibu Spika, Job Ndugai kwenye kikao cha Bunge, mjini Dodoma jana. Picha na Emmanuel Herman

TUNA WAHI BUNGENI

Print
User Rating:  / 0

 

Waziri wa Nishati na Madini, Prof Sospeter Muhongo (kulia) na  Mbunge wa Namtumbo (CCM), Vita Kawawa wakielekea kuhudhuria kikao cha Bunge, mjini Dodoma jana.

TANZANIA BILA UKIMWI INAWEZEKANA

Print
User Rating:  / 1

 

TUMEHITIMU MASOMO YA AWALI

Print
User Rating:  / 0

Baadhi ya wahitimu wa darasa la awali (chekechea) katika Kituo cha Watoto cha Anne Montessori, Mkoani Pwani wakifurahi jambo baada ya kukabidhiwa vyeti vya vyao katika mahafali ya pili ya kituo hicho yaliyofanyika juzi shuleni hapo. Picha na Sanjito Msafiri

NAZINDUA RASMI

Print
User Rating:  / 0

Rais wa Zanzibar, Dk Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuzindua kituo cha Afya kilichopo Kijiji cha Kajengwa, Makunduchi Wilaya ya Kusini Unguja jana, katika shamra shamra za kuadhimisha Miaka 50 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Picha na Ikulu

TUMEPIGA HATUA

Print
User Rating:  / 0

Balozi wa Tanzania nchini Burundi, Dk. James Nzagi (wapili kushoto) akimweleza jambo Aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini humo, Francis Mndolwa (katikati) baada ya kupokea ndege ya Shirika la Ndege la Tanzania, Air Tanzania katika Uwanja wa Ndege wa Kimatifa wa Bujumbura. Na Mpigapicha Wetu

TUTAFIKA TUNAPO PATAKA

Print
User Rating:  / 1

Wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Uyui, mkoani Tabora juzi. Picha na Joseph Senga

AJARI MBAYA DAR

Print
User Rating:  / 6

Wasamaria wema wakiwasaidia majeruhi  kuwapakia kwenye gari tayari kwa kupekwa hospitali baada ya kutokea ajilia ya pikipiki iliyogongana na gari aina Fuso ya katika eneo la Tabata  Tiot , Jijini Dar es S jana. Picha na Juliana Malondo

NISIKILIZENI KWANZA

Print
User Rating:  / 0

 

Waziri wa Nchi, Ofi si ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira (kushoto) akizugumza na Mbunge wa Arumeru Mashariki Joshua Nasari (wa pili kushoto), Mbunge wa Nyamagana, Ezekia Wenje (kulia) na Mbunge wa Musoma Mjini, Vincent Nyerere katika Viwanja vya Bunge mjini Dodoma jana. Picha na Emmanuel Herman

NIMETUMWA NA WANANCHI

Print
User Rating:  / 1

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk Hussein Mwinyi akijibu maswali katika kikao cha Bunge mjini Dodoma jana. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu  ( Uwekezaji na Uwezeshaji), Dk Mary Nagu. Picha na Emmanuel Herman

KIKAO MUHIMU

Print
User Rating:  / 0

 

Wakurugenzi wa halmashauri za wilaya za mkoa wa Lindi wakiwa kwenye kikao cha bodi ya barabara kilichofanyika hivi karibuni chini ya mwenyekiti wa bodi ambaye ni Mkuu wa Mkoa huo, Ludovick Mwananzilah. Na Mpigapicha Wetu

TUNASHUKURU KWA UPENDO WENU

Print
User Rating:  / 0

 

Mkuu wa Polisi wa Dawati la Jinsia, Wanawake na Watoto wa Mkoani Pwani, Yusta Milinga akikabidhi msaada wa vyakula na vifaa vya shule ambavyo dawati hilo liliweza kuungana na kununua ili kuwasaidia watoto yatima na waishio kwenye mazingira hatarishi wa kituo cha Buloma Foundation kilichoko Kibaha Picha ya Ndege, mkoani humo ikiwa ni kuelekea kwenye maadhimisho ya kupinga vitendo vya ukatili kwa makundi hayo mawili ya wanawake na watoto. Picha na Sanjito Msafiri

IPO SIKU MUNGU ATANIONA

Print
User Rating:  / 1

 

NAPUNGUZA UMASKINI NCHINI KWANGU

Print
User Rating:  / 0

 

Mfanyabiashara Emmanuel Jonas akipamba mti ya krisimasi katika eneo la Mwenge Sokoni ambapo alikuwa akiuza kati ya Sh 35,000 na Sh 160,000 kulingana na ukubwa wa mti. Picha na Michael Jamson

MARIA NYERERE VIONGOZI IGENI WEMA WA MANDERA

Print
User Rating:  / 0

 

HATA SISI TUPEWE NAFASI YA KUCHANGIA

Print
User Rating:  / 0

Mbunge wa Viti Maalum, Christowaja Mtinda (katikati) akichangia kwenye warsha ya wabunge walipokuwa wakijadili mafanikio na matatizo ya MKUKUTA, changamoto ya Millenia na Mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN), iliyofanyika Dodoma juzi. Picha na Emmanuel Herman

TULIA NIKUPIGE PICHA MZEE

Print
User Rating:  / 0

 

Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk Makongoro Mahanga akimpiga picha Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu wakati kikao cha bunge kilipokuwa kikiendelea mjini Dodoma jana. Picha na Emmanuel Herman

UZINDUZI WA SANAMU LA MADIBA

Print
User Rating:  / 0

                                                                                                                                                                                     

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Sanamu lenye urefu wa mita 9 la Rais wa Kwanza Mazalendo wa Afrika Kusini, Nelson Mandela likiziduliwa katika Ikulu ya Pretoria nchini humo jana. Picha na AFP

Mahujaji warejea nchini

Print
User Rating:  / 0

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Mmoja wa Mahujaji, Mwajuma Adam akiomba dua na ndugu zake waliokwenda kumpokea  katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  (JNIA) jijini Dar es Salaam jana,  wakati Mahujaji walipokuwa wakirejea kutoka Miji Mitakatifu ya Makkah na Madina.  Picha na Salim Shao

Kuweni makini sana makamanda wangu

Print
User Rating:  / 5

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga, Costantine Massawe (katikati) akionyesha silaha zilizotumika kupambana na Polisi kilindi na kuuawa kwa Salum Mngonje pia kupigwa risasi Mkuu wa Polisi, Inspecta Lusekelo Edward. Picha na Burhani yakub.

Kikao cha hitishwa bungeni

Print
User Rating:  / 0

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Spika wa Bunge Anne Makinda akiongoza kikao cha kamati ya Uongozi kinachoundwa na wenyeviti wote wa Kamati za Bunge Ofisini kwake Bungeni Dodoma kujadili shughuli zitakazokuwemo kwenye ratiba ya Mkutano wa 13 wa Bunge unaotarajia kuanza leo.  Picha na Owen Mwandumbya wa Bunge

Usindikwaji wa dagaa Sokoni Ferry

Print
User Rating:  / 0

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Muuza dagaa katika soko la Ferry Chikaukau Wa Kumunya,akiwaanika dagaa kama njia ya kuwasindika wasiharibike,ambapo huwauza Sh2,500 kwa kilo.Picha na Michael Jamson

Majonzi ya tawala msibani

Print
User Rating:  / 1

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Bi Tunguli Rajabu  ambaye ni mama wa askari mlinda amani aliyefia Congo Luteni Rajabu Mlima, akiwa na majonzi  kwenye  Msiba nyumbani kwao Mbezi Beach Makonde jijini Dar es salaam.Picha na Juliana Malondo

Kilio cha tanda mahakamani

Print
User Rating:  / 2

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Waziri  zamani wa Ofisi wa Makamu wa Rais Mazingira, Arcado Ntagazwa, akifuta machozi huku akitazamwa na mwenzake Senator Miselya baada ya wote wawili na mtoto Ntagazwa, Webhale , kuachiwa na Makahama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam jana, kutokana na kesi iliyokuwa ya kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu. Picha na Emmanuel Herman

Abel Mkubwa achomoka na Mwananchi

Print
User Rating:  / 0

Mshindi wa Chomoka na Mwananchi, Kutoka Mbeya, Abel Mkubwa (kulia) akikabidhiwa mfano wa hundi yenye thamani ya Sh1 milioni, kutoka kwa meneja mauzo na usambazaji wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Nyanda za Juu kusini, Maunde Boniventura.Makabidhiano hayo yalifanyika katika ofisi za MCL Jijini Mbeya. Picha na Godfrey Kahango

Msaada wa jengo

Print
User Rating:  / 1

Meneja Afya, Mazingira na Usalama wa Tanga Cement(TCCL) , Onesmo Kitomari (kulia) akizungumza katika hafla ambayo kampuni hiyo ilikabidhi jengo la madarasa mawili, matundu ya choo na madawati  kwa ajili ya Shule ya Msingi Mangowele Mkoani Mtwara. Hafla ya makabidhiano ilifanyika wakati wa mbio za mwenge wa Uhuru mkoani humo mwishoni mwa wiki.Picha na Abdallah Bakari

Biashara ya madangulo Buguruni

Print
User Rating:  / 6

Mkazi wa Buguruni kwa Madenge jijini Dar es Salaam, Abdul Sungura akionyesha vyumba vinavyotumika kama madanguro baada ya  mkutano wa katika ofisi za Serikali ya Mtaa huo wa  kutatua mgogoro wa suala la kuwepo kwa biashara za madanguro kuahirishwa jana. Picha na Venance Nestory

Mkutano wa hadhara wa CHADEMA Mbeya.

Print
User Rating:  / 3

Katibu Mkuu wa Chadema Taifa, Dk. Willibrod Slaa akiwahutubia wakazi wa  Mbeya mjini  katika mkutano wa hadhara wa chama hicho uliofanyika katika viwanja vya Ruanda Nzovwe Jijini hapo jana kwa lengo la kuwaeleza wananchi kilichomtokea Mbunge wa Jimbo la Mbeya Mjini Joseph Mbilinyi na wabunge wengine bungeni hivi karibuni.

Wabunge hao walitolewa ndani ya ukumbi wa Bunge kwa kile kinachodaiwa kuwa ni ukiukwaji wa Sheria za Bunge hilo. Picha na Godfrey Kahango.

Hali ya Padre aliyemwagiwa tindikali

Print
User Rating:  / 1

Paroko wa Parokia  ya Roho Mtakatifu Cheju Zanzibar, akisaidiwa na Frateri, Richard Haki kupumzika kitandani baada ya kuzungumza na waandishi katika katika Wodi ya Kibasila iliyopo katika Hosipitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijni Dar es Salaam jana. Padre huyo alimwagiwa tindikali na mtu ambaye bado hajatambulika kisiwani Zanzibar. Picha Salim Shao

Uandikiswaji uamiaji Dar es Salaam

Print
User Rating:  / 0

Raia wa Malawi wakijiandikisha katika Idara ya Uhamiaji, Mkoa wa Dar es Salaam jana kutokana na zoezi linaloendelea la kuwatambua wahamiaji haramu jijini Dar es Salaam. Picha  na Felix Mwagara, Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.

Harambee ya kutunisha mfuko wao wa Bima ya Afya

Print
User Rating:  / 2

Watoto wanaoishi katika mazingira hatarishi waliopo katika kijiji cha Mzogole Wilaya ya Bahi wakiwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Betty Mkwasa, mara baada ya kuongoza harambee ya kutunisha mfuko wao wa Bima ya Afya, kushoto kwake ni mkurugenzi wa halimashauri ya Bahi, Rachel   Chuwa. Picha na Noor Shija

Wamepewa walichotaka

Print
User Rating:  / 1

Wananchi wa Misri wakishangilia nje ya Ikulu mjini Cairo baada ya kupata habari Rais Mohammed Morsi wa nchi hiyo jeshi limemvua madaraka yake, juzi. Picha na AFP

Uwajibikaji wa jamii

Print
User Rating:  / 0

Mmoja wa washirki akichangia wakati wa mdahalo unaohusu uwajibikaji wa jamii na ufuatiliaji wa rasilimali za umma katika sekta ya afya wilaya ya Kinondoni juzi, mdahalo huo iliandaliwa na kikundi cha Pakacha Group kwa udhamini wa Shirika la Mfuko wa maendeleo ya jamii. Picha na Salim Shao

Tuyatokomeze jamani!

Print
User Rating:  / 0

Kuluthumu Ramadhani akimsaidia mwanae,  Aziza Mohamedi  mwenye ulemavu wa viungo vya miguu na kuongea kunyonyesha mtoto baada Aziza kujifungua kwa njia ya upasuaji katika hospitali ya wilaya ya kondoa mkoa wa Dodoma kutokana na  ukatili  wa kubakwa. Picha na Shakila Nyerere  

Tunafuatilia jamani!

Print
User Rating:  / 0

Wakazi  wa kijiji cha Unyangwe kata ya Iseke wakisikilza  mgombea Udiwa kwa Tiketi ya Chama cha Wananchi CUF  wakati mkutano wa kampeni katika kata ya Iseke juzi. Picha  na Gasper Andrew.   

Msaada wa walemavu

Print
User Rating:  / 0

Katibu wa jimbo, Parokia  ya Lindi Theophil Mrope  (kushoto )akikabidhiwa chakula  chenye thamani ya zaidi ya Tsh laki tatu na Meneja shirika la hifadhi ya jamii (NSSF) mkoa wa Lindi Hamisi Fakii  (kulia) kwa ajili ya watu wenye ulemavu wanaoishi kituo cha walemavu  Mwenge manispaa ya Lindi jana. Picha na Mwanja Ibadi                                        

CCM oyeee!

Print
User Rating:  / 0

Mgombea kiti cha Udiwani katika uchaguzi mdogo wa Udiwani kata ya Iyela, Jijini Mbeya, Richard Shangwi, (Kulia) kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) akionyesha bendera ya Chama hicho aliyokabihiwa rasimu na Makamu Mwenyekiti wa CCM  Tanzania Bara, Philip Mangula jana ili kuipeperusha kwenye kinyang'anyiro hicho baada ya kuzinduliwa kampeni za chama hicho  Picha na Godfrey Kahango.         

Mafunzo ya wanafunzi kwa vitendo

Print
User Rating:  / 1

Wanafunzi wa shule ya msingi Haydom Wilayani Mbulu Mkoani Manyara wakijifunza kutengeneza nishati ya mkaa mbadala kwenye Kituo cha pembe nne za utamaduni Haydom (4CCP) juzi kwa lengo la kutunza mazingira.Picha na Joseph Lyimo                             

''Tutafika mdogo mdogo''

Print
User Rating:  / 1

Daladala likipita katika njia inayoungnisha Kimara na Bonyokwa nje kidog ya jiji la Dar es Salaam jana, barabara hiyo iliyojengwa kwa kiwango cha changarawe na mifereji mwezi wa tatu kwa sasa inapitika kwa shida baada ya sehemu nyingi kuharibika kutoka na ujenzi kutozingatia utaalumu wa kutosha. Picha na Salhim Shao

''Hatutaki watalii!''

Print
User Rating:  / 0

Wananchi  wanaoishi ndani ya eneo la Mamlaka ya hifadhi ya Ngorongoro katika kijiji cha Olbalbal wakiwa kwenye kikao walichokubaliana kuzuia watalii kuingia katika hifadhi hiyo kwa kufunga geti iwapo serikali haitatekeleza matakwa yao. Picha na Mussa juma

''hali sio nzuri''

Print
User Rating:  / 0

Mvuvi wa samaki kwenye Ziwa Bassotu, mkoa wa Manyara,Charles Manyama akizungumzia hali kipato chao kuyumba baada ya Ziwa hilo kufungwa kwa muda  ili kuwezesha samaki kuongezeka.Picha na Filbert Rweyemamu

Bungeni laendelea

Print
User Rating:  / 0

Mbunge wa Nkasi Kaskazini, Ali Kessy akiwa amefumba mdomo wakati bunge lilipokuwa limekaa kama kamati kupitisha makadirio na matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2013/14, mjini Dodoma jana. Kushoto ni Naibu Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Zitto Kabwe akifurahi wakati Kessy alipokuwa akifanya tukio hilo. Picha na Edwin Mjwahuzi

"Hongera Waziri"

Print
User Rating:  / 1

Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli (mwenye tai nyekundu) akipongezwa na wabunge pamoja na mawaziri baada ya kupitishwa kwa bajeti ya wizara yake kwa mwaka wa fedha 2013/14, mjini Dodoma juzi. Picha na Edwin Mjwahuzi

"Pumzikeni kwa amani"

Print
User Rating:  / 0

Waziri wa Mambo ya Nje wa Canada,John Baird(kushoto)akiweka shada la maua jana kwenye makaburi ya watu watatu waliouawa kwenye tukio la shambulio la bomu kwenye kanisa Katoliki la Mtakatifu Joseph Mfanyakazi Parokia ya Olasiti,jijini Arusha Mei 5,mwaka huu.Picha na Filbert Rweyemamu

Faida za virutubisho katika vyakula

Print
User Rating:  / 1

Ofisa wa Lishe kutoka katika Sekta ya Maendeleo na Menejimenti za Afya, Leticia Chang’a akiwaelezea faida za virutubisho katika vyakula wakazi wa jiji la Dar es Salaaam walitembelea maonesho ya lishe jana  yanayofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja. Picha na Venance Nestory

"Tunalinda mazao"

Print
User Rating:  / 0

Wakulima wa mpunga katika kijiji cha Mgungila mkoani Singida wakiwa kwenye lindo la kuwafukuza ndege ambao wamekuwa wakila mpunga huo, ambapo wamesema bila ya kulinda wanaweza kumaliza shamba lote.Picha na Masoud Masasi

Mkagangamale vijana

Print
User Rating:  / 1

Amiri Jeshi Mkuu Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimkabidhi bendera kiongozi wa batalioni ya  wanajeshi wa JWTZ wanaokwenda  kujiunga na  jeshi la Umoja wa Mataifa la kulinda amani Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, katika sherehe za kuwaaga zilizofanyika Msangani, Kibaha, Mkoa wa Pwani  jana. Picha na Ikulu

Msaada wa blanketi

Print
User Rating:  / 0

Mbunge wa Kishapu mkoani Shinyanga Suleiman Nchambi akikabidhi blanketi kwa waathirika wa mafuriko yaliyotokea katika Vijiji vitatu vya Mwanhili Mwasubi na Itongoitale katika kata  ya Bunambiyu Tarafa ya Mondo  wilayani Kishapu.

Uzinduzi wa ilani ya madai kwa wanawake

Print
User Rating:  / 0

Wananchi wakiwa katika maandamano  jana   kabla ya uzinduzi wa ilani ya madai ya wanawake wa Tanzania katika katiba mpya  iliyotayarishwa na Mtandao wa Jinsia  Tanzania(TGNP) jijini Dar es salaam. Picha na Aika Kimaro      

Ulinzi mkutanoni

Print
User Rating:  / 2

Wakazi wa manispaa ya Singida mkoani humo wakimsikiliza katibu mkuu wa chama cha CUF,Seif Sharrif Hamad katika mkutano wa hadhara uliofanyika juzi.Picha  na Gasper Andrew.

Wanaoperuzi SASA!

We have 33 guests and no members online

Banner One

Popular Blogs